News alert: CIA.gov DDoSed by LulzSec!

Ni kama mchezo unaondelea au vita, leo lulzSec wametangaza kuishambulia tovuti ya CIA, ya marekani. LulzSec wamesema hivyo kwenye account ya twitter. Kama kawaida kila kitu wanachofanya ni kwa ajili ya kujifurahisha. Ni siku chache tu tangu washambulie tovuti ya games [DDoS].

Tovuti ya CIA imekuwa haipatikani na lulz wametanga kuhusika na tukio hilo. Kumekuwa na vijisemo pembeni kwamba wanlenga mashirika madogo madogo, lakini baada ya hapa nadhani ujumbe utakuwa umefika.

READ MORE » News alert: CIA.gov DDoSed by LulzSec!

Steve Jobs akiizindua iCloud

READ MORE » Steve Jobs akiizindua iCloud

iCloud Communications kuishitaki Apple


iCloud ni kampuni VoIP service provider ambao wanaishitaki apple kuharibu ala yao ya kibiashara. Huduma mpya ya Apple ya kuhifadhi muziki kwenye kiwingu imeleta athari kubwa kwenye soko. Vita hivyo vimeanza na apple inabidi ajiandae kupambana navyo wameeleza kwenye tovuti yao [iCloud communications].
READ MORE » iCloud Communications kuishitaki Apple

Tovuti za Serikali [tanzania.go.tz/zanzibar.go.tz] zaongoza njia tovuti mbovu Tanzania

Tovuti ya Tanzania (tanzania.go.tz) ni katika miongoni mwa tovuti zilizokosa mvuto Tanzania. Tovuti imekosa uiano wa rangi katika kurasa zake. Vile vile imejaa viunganishi ambavyo havifanyi kazi, kama hii ambayo imeekwa kwenye kitufe cha 'back' http://www.tanzania.go.tz/index2.html ni kwasababu inajaribu kwenda kwenye amabyo imebadilishwa jina nakuwa 'index2E.html'.
Tovuti ya Zanzibar ni moja ya tovuti ambazo zipo katika hatari ya kuangushwa wakati wowote. Tovuti inakurasa za PHP ambazo zimejaa hitilafu za PHP (php bugs). Kurasa hizo zinaweza tendwa kirahisi, kwasababu zinaonyesha majina ya mafile. Kwa kifupi unaweza kuhack kirahisi.


Na mtu akipata hivyo kinachofata ni kuwa hacked. Kama ifuatavyo:


Ni ombi letu [tungule.com], tovuti ya serikali ya Zanzibar ifungwe iliirikebishwe kabla haijavamiwa. Na ile ya Tanzania, irekebishwe ili iwe na manufaa na iwe ya kutumika.
READ MORE » Tovuti za Serikali [tanzania.go.tz/zanzibar.go.tz] zaongoza njia tovuti mbovu Tanzania

Samsung 5 series wa kwanza Chrome OS [Chromebook]

Samsung 5 series ndio wa kwanza kuzalisha 'Chromebooks'. Ni Laptops (bado tunatafuta tafsir yake,btty), ambazo zinatumia cloud-based Operating system. Laptops hizo zitakuwa zinatumia sekunde chache kuboot, na kuzimika mara moja. Software zote zitakuwa zinapatikana katika tavuti (web), tatizo la kuinstall software na kuifanya kompyuta kuwa slow linaondoka



Hata hivyo Chrome OS inahitaji upatikanji wa uhakika wa intaneti. Kwa Tanzania kwa watu wengi internet ni maofisini na wachache inapatikana nyumbani. Vilevile, inahitaji internet ambayo ni inspidi ya kutosha. Jee Watanzania wangapi watakuwa tiyari kuacha kutimia OS za kawaida na kutumia Chrome. Jee ukienda kwenye ambayo internet haipatikani kabisa?
READ MORE » Samsung 5 series wa kwanza Chrome OS [Chromebook]

Lulz hacks again! this time is a porn site

Kikundi cha mahacker wanaojiita LulzSecurity kimehack tovuti ya ngono na kuziachia email za watumiaji wake mtandaoni. Hio imepelekea watu kujaribu email za watumiaji hao Facebook, hali iliopelekea facebook kuziblock email zote kwenye listi ili watu wasizijaribu email hizo. Ni fundisho kwa wale wanaotumia password moja kwa 'account' zote!



Kikundi hichi kimekuwa kikihack kwa ajili starehe na sio kwa ajili ya pesa. Kama neno lenyewe linvyojieleza,'lulz', ambayo inamanisha wapo kwa ajili ya kujifurahisha.
READ MORE » Lulz hacks again! this time is a porn site

Unalipi la Kusema: Facebook face recognition!

Facebook sasa imeeka teknolojia ya kutambua sura za watumiaji katika picha. Hii itarahisisha kazi ya 'tag' watu katika picha na pia itaimarisha facebook katika swala zima la 'kushare' picha. Facebook ni mtandao unaongoza katika upande wa 'kushare' picha na hivi karibuni imepata hati ya kumiliki 'tagging system' inaotumika katika kushare picha.

Hata hivyo, baado kuna maswali  ya kujiuliza kama swala zima la 'privacy'. Jee teknolojia hii itakuwa na athari gani kwa watumiaji, na vipi itapokelewa. Lakini swali la kujiuliza, maoni yako wewe binafsi, unalichukuliaje swala zima la teknolojia hio.
READ MORE » Unalipi la Kusema: Facebook face recognition!

Playstation Vita official trailer!

 
READ MORE » Playstation Vita official trailer!

Jifundishe kupiga gita leo!





Ingia kwenye mtandao wa google.com na uchezee gita la bandia.
READ MORE » Jifundishe kupiga gita leo!

UN yasema Internet ni haki ya binaadamu

Baada ya matukio kusini mwa Afrika na Mashiriki ya kati, upatikanaji wa internet ni moja mwa haki za binaadamu kwa sasa. Internet imekuwa ni moja mwa kitu muhimu katika maisha ya watu kila siku. Mitandao kama kama Facebook na youtube imedhihirisha hilo kwa kuwa na watumiaji wengi wanaofikia mamilioni.

Hii itatoa changamoto kwa nchi kama ya Tanzania kuboresha huduma ya internet ambayo upatikanaji wake ni wa ghali sana. Ikiwa ni miaka michache tangu tujiunge na mkonga, bado marekebisho yanahitajika katika ugawaji wa huduma hio.
READ MORE » UN yasema Internet ni haki ya binaadamu
 
© 2010 tungule | Blog Theme