Uwezekano:Nishati mbadala

‘Gongo’ ni aina ya pombe ambayo imepigwa marufuku nchini Tanzania. Kwa hakika, kuna madhara mengi yaliowahi tokea ambayo yamesababishwa na pombe hio. Kiutaalam, ‘gongo’ ni ‘Ethanol’. Ethanol imethibitisha kuwa ni nishati mbadala ambayo ni fanisi hasa kwa vyombo vya barabarani. Baadhi ya nchi zimekuwa zikitumia ‘ethanol’ hasa kwa usafiri wa umma. Sio tu ni nishati fanisi, bali pia inasifika kwa kutunza mazingira na kuwa madhara kidogo kwa hewa (“low carbon emmissions”).

Kutokana na maelezo hapo juu na kutokana na gharama za juu za usafiri nchini (angalia SUMATRA), ni wazi kwamba huu ni wakati wa kushirikiana na wapika gongo ili iwe inatumika kwa njia zinazofaa na kunafaisha. Wakina mama wanaopika gongo wakiwekewa ‘standards’ za kufuata na wakipewa ruzuku za kuwaezesha kufanya kazi, itasaidia kuzalishwa ‘ethanol’ nyingi. Ethanol ikipatikana nyingi na ya kutosha, nadhani ni wazi kwamba ni wakati wa kubadilika na kuanza ‘ethanol’ kwenye madaladala na mabasi ya miji badala ya kutumia petroli ambayo ni ghali na ambayo inamwaga uchafu mwingi kwenye hewa.

[caption id="attachment_163" align="aligncenter" width="500" caption="Ethanol Powered Bus (NCTX)"]eb[/caption]

Faida ni nyingi, sio tu kutunza mazingira bali tutakuwa mfano kwa mataifa mengine ya Afrika. Bei za usafiri wa mijini itashuka kupelekea kupungua kwa gharama ya maisha mijini. Pia, akina mama ambão walikuwa wakiwindwa na vyombo vya sheria kwakutengeza pombe hii haramu, watakuwa wameweza jipatia ajira ambayo itakuwa msaada tosha kwa wao na kwa nchi kwa ujumla.

Hata hivyo, kuacha kutumia petroli na kuanza kutumia ‘ethanol’ ni vigumu mno. Kwanza, wazo hili litarajie kupata kipangimizi kikubwa kutoka kwa wamiliki wa masheli amabao upunguzi wa bei za mafuta ni kikwazo kwa wao si kwambii mada husika. Vilevile kisiasa ni maamuzi magumu kufanya katika nchi kutokana na athari kwa baadhi ya wafanya biashara wakubwa nchini.

Kwa kumalizia, faida za ‘ethanol’ ni nyingi, na kwa kuzingatia hali ya sasa, ni wakati wa kuanza kufanya utafiti ili tujikomboe kama nchi. Japokuwa kutakuwa na vipangamizi katika kuezesha uhamiaji huo, lakini faida zake ni muhimu sana. Ikiwa kweli tunataka kuwapunguzi wananchi ugumu wa maisha, basi jee hatuoni kwamba tunahitaji kuangalia nishati hii mbadala?

0 comments:

Post a Comment

 
© 2010 tungule | Blog Theme