Teknolojia mpya ni ngumu bila umeme!

Tatizo la umeme ni kikwazo kwa watanzania hasa wanaotaka kubadilisha hali ya Teknolojia nchini. Nashindwa kuelewa, ni asilimia ngapi ya watanzania wanaishi bila ya umeme. Kilicho tokea Zanzibar ni aibu na tena jambo la kukatisha tamaa; mara mbili ndani ya miaka miwili. Au labda tujiulize kwa wale wanaopata umeme ni asilimia ngapi ya muda wa maisha yao wanakosa umeme? Uzalishaji wa umeme wa kutosha Tanzania ni muhimu kwa watu wake na kwa Taifa kwa ujumla.

Kwa kuongezea, ni kama uaji wa wafanya biashara ndogo ndogo. Sasa ndio wakati wa kulivalia njuga swala la umeme ili kukuza teknolojia na kukuza uekezaji. Wangapi wamekatisshwa tamaa kuwasilisha mawazo yao kisa sababu ya upatikanaji mdogo wa umeme. Pia, kazi ngapi zimeharibika baada ukatikaji wa ghafla wa umeme? Cha kushangaza nchi yetu inasifika kwa kuwa ya kijani, na huku hali ya nchi inalazimisha utumiaji wa majenereta yaanaochafua mazingira! Binafsi, sijwahi sikia nchi inaendelea kwa mgao wa umeme!

Kwa kumalizia, ni wazi kwamba uzalishaji wa umeme ni ishara tosha inayoashiria jinsi gani  nchi ipo makini katika kuhakikisha swala zima la maendeleo. Maendeleo bila umeme unaokidhi mahitaji na unaopatikana saa zote  ni ngumu. Wanasiasa wanajukumu, na jukumu lao kuhakisha wanasayansi wanaisaidia nchi yao na huu ndio wakati. Tunahitaji uzalishaji wa umeme na mgao sasa iwe basi.



[caption id="attachment_113" align="aligncenter" width="540" caption="Mh. William Mganga Ngeleja - World Economic Forum on Africa 2010"][/caption]

1 comments:

kibabu said...

Kweli kabisa Tungule maana hali hii inavyozidikuendelea ndio tunazidikurudi nyuma kimaendeleo.mgao sasa basi na wadau wa sekta binafsi jitokezeni ili muwasaidie watanzania wenzenu jamani mara ngapi umeme unakatwa wakati operesheni zinaendelea mahospitali? vifo vingapi vimeshasababishwa na ukataji huu wa umeme? tuamkeni watanzania.
mdau

Post a Comment

 
© 2010 tungule | Blog Theme